Home Sports AZAM FC YATUNGULIWA SOPU AKITUPIA MBILI

AZAM FC YATUNGULIWA SOPU AKITUPIA MBILI

DAKIKA zake 71 zilitosha kufanya ubao wa Uwanja wa Mkapa ukasoma Azam FC 2-3 Yanga.

Ni Abdul Seleman, ‘Sopu’ nyota wa Azam FC alikuwa kwenye ubora lakini timu yake ya Azam FC imetunguliwa ikiwa nyumbani na kuyeyusha pointi tatu mazima.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele dakika ya 31 na Aziz KI dakika ya 32 huku lile la ushindi likifungwa na Farid Mussa.

Kiungo Farid aliingia kipindi cha pili akitokea benchi na kuipa timu hiyo matokeo chanya.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Azam FC ikiwa ugenini ilikubali sare ya kufungana mabao 2-2, leo ikiwa nyumbani imenyooshwa jumlajumla.

Unakuwa mchezo wa Kali Ongala kuonja ladha ya kufungwa baada ya kukaimu nafasi ya kukinoa kikosi cha Azam FC.

Previous articleALI AHAMADA ATUNGULIWA MBILI CHAP KWA HARAKA
Next articleEPL KUTIMUA VUMBI KUANZIA LEO BOXING DAY, ODDS NI BOMBAA! MERIDIANBET