Home International MESSI KABEBA TAJI, MBAPPE KAWEKA REKODI

MESSI KABEBA TAJI, MBAPPE KAWEKA REKODI

NYOTA Lionel Messi aliiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa kuwashinda mabingwa watetezi Ufaransa kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya 3-3 ndani ya dakika 120.

Katika mchezo huo ambao utaingia kwenye historia ya kuwa miongoni mwa mchezo mkubwa wa fainali kupata kuchezwa kwa vigogo hao wawili Uwanja wa Lusail Iconic.

 Ufaransa walitoka nyuma mara mbili wakipindua meza jambo lililofanya mchezo huo mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penalti.

Licha ya kwamba Messi atachukuwa vichwa vya habari, Kylian Mbappe alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwenye fainali ya Kombe la Dunia tangu Sir Geoff Hurst akiwa na England kufanya hivyo  mwaka 1966.

Argentina walitawala kwa dakika 80 za mwanzo na walionekana kujiandaa kunyakua taji lao la kwanza la Kombe la Dunia tangu 1986. Messi aliifungia timu yake mkwaju wa penalti dakika ya 23 baada ya Ousmane Dembele kuhukumiwa kumkwaa Angel Di Maria.

Winga wa Juventus Di Maria aliiongezea Argentina bao la pili baada ya kuwa kwenye spidi kwa kuongozwa na pasi elekezi ya Alexis Mac Allister wa Brighton  huku Ufaransa ikionekana kukabiliwa na madhara ya ugonjwa kambini.

Ni dakika ya 79 baada ya Randal Kolo Muani kuangushwa na Nicolas Otamendi Mbappe alifunga bao lake la kwanza jioni, kabla ya kuongeza la pili sekunde 90 baadaye na kupeleka mchezo kwenye muda wa ziada.

Mbappe alifunga bao la kwanza dakika ya 80 na lile la pili dakika ya 81 ikiwa ni muda mfupi wa kutengenanisha ubingwa kwa mchezaji mwenzake anayecheza naye PSG Messi.

Messi alidhani ameshinda kwa upande wake huku bao lake la pili lilitolewa na teknolojia ya mstari wa goli katika dakika ya 108. Lakini, zikiwa zimesalia dakika chache za mchezo, Ufaransa walipata penalti nyingine baada ya Gonzalo Montiel kuonekana akishika mpira kwa mkono kwenye harakati za kuokoa.

Mbappe aliongeza kwa mara ya pili na kwa mara nyingine kumpiga Emiliano Martinez, na kuwafanya Ufaransa kurejea kwenye sare kwa mara ya pili na kupeleka mchezo kwenye mikwaju ya penalti.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alifunga bao lake la tatu jioni  kabla ya Messi kujibu.

Lakini Kinsgley Coman na Aurelien Tchouameni wote walikosa mikwaju yao ya penalti kwa Ufaransa huku Argentina ikifunga kila moja kati ya matatu yaliyosalia, huku Montiel akipiga mkwaju wa penalti wa ushindi na kushinda Kombe la Dunia la 2022.

Tags # Kimataifa

Previous articleKOCHA COASTAL UNION MAMBO MAGUMU
Next articleVIDEO:MANZOKI KUTUA SIMBA/GADIEL, NYONI KUSEPA