FEI, MAYELE KUIBUKIA POLISI TANZANIA

CEDRICK Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema moja ya sababu iliyowafanya wasitumie wachezaji wote kwenye mchezo wao dhidi ya Kurugenzi FC ni kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi kwenye mchezo wa raundi ya Pili Kombe la Shirikisho waliibuka na ushindi wa mabao 8-0 huku mshambuliaji Clement Mzize akitupia mabao manne.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikosa mchezo huo ni pamoja na kiungo Feisal Salum,Fiston Mayele, Tuisila Kisinda huku Yusuph Athuman na David Bryson wakiwa ni miongoni mwa nyota waliocheza mchezo huo.

Kaze amesema :”Kuna wachezaji ambao hatukuwatumia kwenye mchezo dhidi ya Kurugenzi ikiwa ni kwa ajili ya kubadilisha kikosi pamoja na kuwapa muda kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania.

“Tunaamini utakuwa mchezo mgumu lakini ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu,” .

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Desemba 17,2022 Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.