KLABU ya Yanga, imepangwa kundi moja na timu za TP Mazembe ya DR Congo, US Monastir ya nchini Tunisia na Real Bamako ya Mali katika droo iliyofanyika hii leo.
Yanga inayoshiriki katika Ligi ya Shirikisho Barani Afrika, ilifuzu kuingia katika hatua ya makundi baada ya kung’ara katika hatua za awali ambapo sasa, wamepangwa katika Kundi D.