KLABU ya Simba ya Tanzania, imepangwa katika kundi C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Kwenye kundi hilo ambalo ikiwa Simba watapanga kete vizuri wanaweza kutusua na wakibugi watapotezwa itakutana na Vipers kutoka Uganda, Horoya ya Guinea na Raja Cassablanca ya Morocco.
Simba ilifanikiwa kuingia katika Hatua ya Makundi katika mashindano ya Klabu Bingwa na sasa itakuwa na kazi ya kupambana na miamba hiyo, ili kusonga mbele.
Kazi kubwa kwa wawakilishi hao ni kusaka pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza jambo litakalowapa tiketi ya kusonga mbele.