Home Sports BINGWA MPYA WA TFF BONANZA APATIKANA

BINGWA MPYA WA TFF BONANZA APATIKANA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amewakabidhi Kombe Mabingwa wa 3rd TFF Media Day Bonanza 2022 Uhuru Media na kuweka wazi kuwa wakati ujao kutakuwa na maboresho zaidi.

Uhuru Media imepata ushindi huo kwa kuwatungua bao 1-0 Online Media kwenye Bonanza ambalo limefanyika Uwanja wa Gwambina.

Moja ya fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja kutokana na timu zote kuwa na hesabu za kutwaa ubingwa huo.

Mabingwa ambao walikuwa wanatetea taji hilo walikuwa ni TFF waliondolewa na Wapo Media iliyoondolewa na Uhuru Media.

Onlinde Media ilianza kwa kupata ushindi mapema wa penalti 5-4 dhidi ya Global Publisher

Previous articleSIMBA KAMILI KUVAANA NA WAJEDA, REKODI ZAO ZINAWATESA
Next articleVIDEO:MASHABIKI YANGA WAGOMEA SIMBA KUMSAJILI MANZOKI