Home Sports SIMBA KAMILI KUVAANA NA WAJEDA, REKODI ZAO ZINAWATESA

SIMBA KAMILI KUVAANA NA WAJEDA, REKODI ZAO ZINAWATESA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wake Eagle kwenye mchezo wa raundi ya Pili Kombe la Shirikisho yapo tayari.

Hawa ni Wajeda wanakabiliana na Simba ambayo iliukosa ubingwa huo mwaka jana 2021 na mabingwa walikuwa ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Simba haijawa na mwendo mzuri kwenye hatua ya raundi ya Pili Kombe la Shirikisho inapokutana na timu za Wajeda.

Ikumbukwe kwamba Simba ilipoteza mbele ya Green Warriors kwa mikwaju 3-4 ya penalti baada ya ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Simba 1-1 muda wa kawaida.

Ngoma ilirudia tena mbele ya Mashujaa ilipopoteza kwa kufungwa mabao 2-3, Uwanja wa Mkapa zama za Patrick Aussems.

Leo Desemba 10,2022 ni Simba v Eagle, Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa wachezaji wa Simba amao walikuwa kwenye mazoezi ya mwisho Desemba 9,2022 ilikuwa ni pamoja na Jonas Mkude, Henock Inonga, Erasto Nyoni.

Previous articleISHU YA KIUNGO MGANDA KUGOMEA MKATABA YANGA IPO HIVI
Next articleBINGWA MPYA WA TFF BONANZA APATIKANA