Home International KULE QATAR KUNA LAKUJIFUNZA KWETU PIA

KULE QATAR KUNA LAKUJIFUNZA KWETU PIA

UNAONA namna ushindani ndani ya Kombe la Dunia na kila timu inafanya kweli kupata matokeo baada ya dakika 90 kukamilika?

Hakika kuna jambo ambalo lipo kwenye mashindano haya makubwa na kila mmoja anafanya kazi yake kutimiza majukumu yae.

Umependa namna Korea Kusini inavyocheza kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo wao mmoja wakiwa hawana mambo mengi ndani ya uwanja?

Hujapenda kuwaona Wajapan wakisaka mpira katika Kombe la Dunia huko Qatar 2022, bado hujapata jambo hapo kutokana na kasi yao licha ya kugotea njiani?

Kwenye vichwa vyao akilini mwao neno kushindwa halipo hata kama wanakutana na ugumu kiasi gani hasa wanapohitaji kufikia mafanikio ambayo wanahitaji.

Muda ni sasa wa kujifunza kutokana na kile ambacho wanakifanya kutoka huko mbele na sasa kuhamia kwenye akili zetu katika utendaji.

Umeona makosa ambayo wachezaji wetu kutoka Afrika wanafanya namna ambavyo yanafanana kwenye kila mchezo?

Unadhani kwa nini inakuwa hivyo kwetu kila siku, wale unaowapa nafasi ya kufanya vizuri wanazingua na wale ambao huwatarajii wanakupa kitu ambacho hukitarajii, lazima kuwe na mabadiliko wakati ujao.

Ghana, unadhani walikuwa wamekosa nini mpaka kugotea kwenye nafasi ya makundi Kombe la Dunia Qatar licha ya kuwa kwenye mwendo mzuri, kuna la kujifunza pia.

Cameroon mchezo mzuri walioonyesha mbele ya Brazil na kupata ushindi mwanzo walikuwa wamekwenda wapi ama walidhani kwamba wapo peke yao kwenye mashindano hayo?

Yote kwa yote timu kutoka Afrika zimeonyesha namna ambavyo zinaweza kuwapa kitu mashabiki na kufanya kweli kweye mechi zote.

Ukweli ni kwamba kila wachezaji ambao wanapata nafasi kwenye mechi katika Kombe la Dunia wanajitoa kwa asilimia 100 bila kujali aina ya timu ambayo inacheza.

Kwa kila timu hapa tunaona kwamba malengo makubwa kwenye mechi ambayo wanacheza wanakubaliana kucheza bila kuogopa na hili ni jambo la kujifunza.

Nina amini kwamba wachezaji wazawa wanapata muda wa kutazama namna wapinzani wanavyopata upinzani kwenye mechi ambazo wanacheza.

Hakuna ambaye anakubali kuona anashindwa hata kama watakuwa wamepoteza mchezo kipindi cha kwanza ama kipindi cha pili.

Muda wote wanajipanga na kuanza upya kama hakuna kilichotkea na mashabiki wamekuwa wakishangilia muda mwingi hili ni jambo lingine.

Kwa maana hiyo mashabiki wana kitu cha kujifunza na wachezaji wana kitu cha kujifunza kwenye hili Kombe la Dunia Qatar.

Wapo ambao wamekwenda kutazama namna gani wengine wanacheza na wengine wamekwenda kutazama mpira na mazingira.

Muda mzuri wa kujifunza kwa wakati mwingine kwenye mechi zijazo ikiwa wameshindwa na wale ambao watakuwa na muda wa kujipanga kwa mechi zijazo ni muhimu kuendelea kufanya kazi nzuri.

Hakika ukweli ni kwamba ushindani ni mkubwa na unavutia kwa kila timu kuingia uwanjani kusaka ushindi na hili linaleta kitu kizuri.

Wachezaji mmeona namna wachezaji wengine ambao wanafanya kazi kutafuta ushindi bila kukata tamaa na mwisho matokeo yanapatikana.

Pongezi kwa wale ambao wanajifunza jambo kupitia Kombe la Dunia iwe hivyo hata watakapokuwa kwenye mechi zao za ushindani uwanjani.

Kila kitu kinawezekana kutokana na mipango ambayo inapangwa ndani ya dakika 90 hakuna kazi nyepesi kwenye kusaka ushindi.

Iwe unashabikia Ghana, Cameroon, Morocco ama Brazili au mabingwa watetezi Ufaransa ninaona mmeona namna ushindani ulivyo.

Hapa hakuna timu yenye uhakika asilimia 100 kusepa na ubingwa kutokana na namna ambavyo wapinzani wanafanya maandalizi yao.

Hakika ni wakati mzuri wa kujifunza na kufanya vizuri kwa wakati ujao.

Previous articleMZUNGUKO WA KWANZA SOMO KWA WALIOKOSA NAFASI
Next articleYANGA NDANI YA LINDI,KUIKABILI NAMUNGO