MZUNGUKO WA KWANZA SOMO KWA WALIOKOSA NAFASI

HAKUNA ambaye anapenda kukaa benchi kwenye mechi ambazo zinaendelea kwa kuwa mchezaji kazi yake kubwa ni kutumia dakika 90 uwanjani.

Imekuwa hivyo kwenye mzunguko wa kwanza ambapo wapo wachezaji waliokwama kuwa kwenye chaguo la kwanza la kocha.

Benchi la ufundi linahitaji wachezaji ambao wanajitoa muda wote kutafuta ushindi na haya yote yanayotokea kwenye mechi lazima iwe ni somo.

Kwa mchezaji ambaye alikosa nafasi kikosi cha kwanza wakati huu ni kujipanga upya kwa mzunguko wa pili ili afanikishe malengo ya kupata namba.

Kitu pekee ambacho kitampa namba mchezaji kikosi cha kwanza ni juhudi zake mazoezini na kufanya kweli kwenye mechi ya ushindani.

Tofauti na hapo ni ngumu kwa mchezaji kupata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na muda mwingine hata kukaa kwenye benchi nafasi hapati.

Kwa muda ambao umepita hasa kwenye mechi za mzunguko wa kwanza wachezaji wamepata funzo namna ambavyo benchi la ufundi linahitaji.

Ule mfumo ambao anahitaji mwalimu utakuwa umeaanza kukaa kwenye vichwa vya wale wachezaji ambao walikuwa hawana nafasi.

Ikiwa walipata nafasi wakashindwa kuzitumia kuna kitu watakuwa wamepata hivyo mzunguko wa pili utakuwa na mabadiliko makubwa kwenye kila idara.

Ikumbukwe kwamba mzunguko wa pili ni muda pekee uliobaki kwa wachezaji kupata nafasi ya kubaki ndani ya kikosi hicho ama kuondoka.

Pia ni muda ambao utafungua ukurasa kwa timu zao kushinda mataji ambayo wanashindania muda ni sasa na inawezekana.

Tags # makala

About Dizo One

makala

NO COMMENTS:

POST A COMMENT

Older Post

Social

Sponsor

Tags

About Us

Contact Form

Name
Email *
Message *