Home Sports MRITHI MIKOBA YA MKWASA ATANGAZWA

MRITHI MIKOBA YA MKWASA ATANGAZWA

 UONGOZI wa Klabu ya Ruvu Shooting umemtangaza Kocha Mkuu Mbwana Makataa ambaye atakuwa ndani ya kikosi hicho kwa sasa.

  Ni mkataba wa mwaka mmoja amepewa akibeba mikoba iliyoachwa wazi na Charles Boniface Mkwasa ambaye ajiuzulu nafasi yake hapo jana, Desemba 5,2022 kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo katika mzungumko wa kwanza wa ligi kuu ambao umemalizika hivi karibuni.

Mkwasa mchezo wake wa mwisho kukaa kwenye benchi la ufundi timu yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji, timu ambayo Makata aliwahi kuifundisha.

Timu yake ya mwisho kuinoa Makata ilikuwa ni Mbeya Kwanza iliyoshuka daraja ambapo aliwahi kukutana na adhabu ya kufungiwa miaka mitano.

Adhabu hiyo ilipunguzwa kutokana na Makata kuomba msamaha kwa makosa ambayo aliyafanya jambo lililopelekea akapunguziwa adhabu hiyo.

Previous articleHUYU HAPA MCHEZAJI BORA YANGA V PRISONS, ALIKIWASHA
Next articleMZUNGUKO WA KWANZA SOMO KWA WALIOKOSA NAFASI