Home Sports POLISI TANZANIA YAMTAMBULISHA KOCHA WA YANGA

POLISI TANZANIA YAMTAMBULISHA KOCHA WA YANGA

MWINYI Zahera aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga ametambulishwa kuwa Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na uongozi wa Polisi Tanzania umebainisha kuwa umefikia hatua hiyo baada ya kuwa na mazungumzo ya muda mrefu na kocha huyo.

Msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, Polisi Tanzania haijawa kwenye mwendo mzuri ambapo mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

Uongozi wa Polisi Tanzania umewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa bega kwa bega na kocha huyo kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

Kwenye msimamo Polisi Tanzania ipo nafasi ya 16 ikiwa imekusanya pointi 9

Previous articleMOROCCO WAPETA, UBELGIJI MAJANGA
Next articleAZAM FC HESABU KWA POLISI TANZANIA