Home International MOROCCO WAPETA, UBELGIJI MAJANGA

MOROCCO WAPETA, UBELGIJI MAJANGA

MWAMBA Hakim Ziyech nyota wa timu ya taifa ya Morocco alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo wakati timu hiyo ikiibamiza mabao 2-1 timu ya taifa ya Canada.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Al Thumama mbele ya mashabiki 43,102 Canada walifungashiwa virago mazima wakigotea nafasi ya nne.

Bao ambalo walilipata ilikuwa ni kupitia kwa nyota Nayef Aguerd ambaye alijifunga dakika ya 40 yale ya Morocco yalifungwa na Hakim Ziyech dakika ya 14 na Youssef En Nesryi dakika ya 23.

Ushindi huo unaifanya Morocco kutoka Afrika kumaliza kundi F ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 7 wanaungana na Croatia ambayo imemaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye kundi na pointi zao ni tano.

Morocco inatinga hatua ya 16 bora baada ya kuyeyuka miaka 36 mchezo wao ujao watacheza na Hispania Uwanja wa Al Rayyan, Jumanne.

Wakati Croatia wakitoshana nguvu bila kufungana na Ubelgiji muda mfupi baadaye, Kocha Mkuu wa Ubelgiji ambaye ametengeneza kikosi cha dhahabu alibangwa manyanga.

Kwenye mchezo huo Ubelgiji yenye Romelu Lukaku alikosa nafasi ya wazi kuipa ushindi timu hiyo jambo ambalo limewapa makasiriko mashabiki wa Ubelgiji ila ni maisha ya mpira.

Canada imamaliza ikiwa nafasi ya nne kwenye kundi F haijakusanya pointi, Croatia nafasi ya pili inaungana na Tunisia hatua ya 16 bora Kombe la Dunia 2022, Qatar.

Previous articleKIUNGO AOMBEWA ULINZI YANGA HUYU HAPA
Next articlePOLISI TANZANIA YAMTAMBULISHA KOCHA WA YANGA