Home Uncategorized YANGA YAIPIGA 4G SINGIDA BIG STARS

YANGA YAIPIGA 4G SINGIDA BIG STARS

FISTON Mayele nyota wa Yanga amefikisha mabao 6 kibindoni baada ya leo kufunga hat trick kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars.

Dakika 90 zimekamilika kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 4-1 Singida Big Stars ikiwa ni ushindi mkubwa kwa Yanga kuupata wakiwa nyumbani msimu huu.

Bao lingine la Yanga limefungwa na beki Kibwana Shomari ikiwa ni bao lake la kwanza kwa msimu huu wa 2022/23.

Kwa Singida Big Stars ni Meddie Kagere alimtungua Aboutwalib Mshery na kuiandikia bao la kufutia machozi Singida Big Stars.

Yanga inafikisha pointi 26 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimmo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 10 inaishusha Azam FC nafasi ya pili huku watani zao wa jad Simba wakiwa nafasi ya tatu.

Previous articleSIMBA YAMTAMBULISHA KOCHA WA VIUNGO
Next articleKMC NA MERIDIANBET WACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI