Home International CR 7 KUVUNJIWA MKATABA MAN U

CR 7 KUVUNJIWA MKATABA MAN U

UONGOZI wa Manchester United umeweka wazi kuwa uko tayari kuvunja mkataba wa staa wao raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo.

Sababu hiyo inakuja kutokana na staa huyo kuikosoa timu hiyo kupitia mahojiano ya moja kwa moja ya kipindi cha Talk TV cha mwandishi, Piers Morgan.

Kwenye kipindi hicho Ronaldo alitoa tathmini nzito kuhusu Manchester United huku akiweka wazi kuwa hamheshimu kocha wake, Erik ten Hag.

Akizungumza kuhusu hilo rafiki wa karibu wa Ronaldo, Rio Ferdinand alisema:”Huwezi kuteteta kile kilichotokea, sioni kama kuna njia yoyote ya kurudi, sihisi kama klabu itamrudisha na wala sidhani kama yeye mwenyewe anataka kurudi. Naamini hii yote imetengenezwa ili aondoke,”.

Uongozi wa United ulitoa taarifa rasmi ya sakata hilo iliyoeleza:”Kwa sasa lengo letu kuu linabaki kuwa katika maandalizi ya nusu ya pili ya msimu kuendeleza kasi, imani na umoja unaojengwa kati ya wachezaji, meneja,wafanyakazi na mashabiki,”

Previous articleHII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA
Next articleVIDEO:USAJILI SAFU YA USHAMBULIAJI SIMBA MGUNDA AFUNGUKA