Home Sports UKUTA WA SIMBA NGOMA NGUMU KWENYE LIGI

UKUTA WA SIMBA NGOMA NGUMU KWENYE LIGI

UKUTA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda umekuwa ni kama chuma kutokana na kuruhusu mabao machache.

Simba ikiwa imecheza mechi 8 ambazo ni dakika 720 imeokota nyavuni mabao manne ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 180.

Ni Joash Onyango, Henock Inonga, Mohamed Hussein,Shomari Kapombe hawa ni baadhi ya wanaounda ukuta wa Simba.

 Safu ya ushambuliaji imetupia mabao 17 na kinara ni Moses Phiri mwenye mabao matano na pasi moja ya bao.

Mabao yote ambayo ameyafunga Phiri katupia kwenye Uwanja wa Mkapa kwa kuzifunga timu tano tofauti hivyo mwendo wake ni mojamoja.

Kipa namba moja Aishi Manula amekaa langoni kwenye mechi zote 8 akiyeyusha dakika 720 hajafungwa kwenye mechi tano msimu wa 2022/23.

Ukuta huo umekuwa ni ngoma ngumu kupenywa na wapinzani kwenye mechi za ligi ukiwa unaongoza kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache kwenye ligi.

Previous articleVIDEO:HUYU HAPA ALLY KAMWE WA YANGA AWATULIZA MASHABIKI
Next articleVIDEO:MASTAA 21 YANGA WAKWEA PIPA/HAKUNA KUJILINDA KAZIKAZI