Home Uncategorized MAYELE:MSITUKATIE TAMAA INAWEZEKANA

MAYELE:MSITUKATIE TAMAA INAWEZEKANA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa kwani bado wanayo nafasi nzuri ya kufanya vizuri wakiwa ugenini.

Nyota huyo amewaomba mashabiki wasiwakatie tamaa kwa kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya leo ambayo ni ya marudio.

Yanga wameshindwa kutamba katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Al Hilal kutoka Sudan.

 Mayele amesema kuwa, bado safari ya kwenda makundi haijamalizika kwani wanao uwezo wa kusonga mbele wakiwa ugenini huku akiwataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwapa moyo wa kupambana.

“Mashabiki tunajua jinsi gani walivyoumizwa na matokeo ya sare tukiwa nyumbani, na kwa kiasi kikubwa tunafahamu kuwa haikuwa matarajio yetu kupata sare.

“Tunawahakikishia mashabiki wetu kuwa tutapambana katika mchezo ujao ambao tutakuwa ugenini kuhakikisha kuwa tunaibuka na matokeo, tunawaomba mashabiki wasitukatie tamaa,” amesema mshambuliaji huyo.

Previous articleMASTAA WATATU MSIMBAZI KUIKOSA de AGOSTO
Next articleHIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA V de AGOSTO