Home Sports NABI: SISI HATUONGEI SANA NI KUTAFUTA MATOKEO

NABI: SISI HATUONGEI SANA NI KUTAFUTA MATOKEO

 NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo wao wa kesho utakuwa mgumu lakini wao hawaongei sana zaidi ni kutafuta matokeo.

Yanga itawakaribisha Al Hilal kwenye mchezo wa raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo amebainisha kuwa maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa imani ya kupata matokeo kwenye mchezo wao.

“Sisi hatuongei sana tunakwenda kufanya kazi suala la kuongea tumewaachia mashabiki kwa sababu tunajua wanachokitaka siyo maneno ni matokeo mazuri na tumejiandaa kufanya vizuri.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuisapoti timu yao uzuri ni kwamba kila mchezaji anatambua namna ilivyo na ushindani utakuwa mkubwa,” amesema.

Previous articleMETACHA MNATA AWAPONZA SINGIDA BIG STARS
Next articleWATATU WA SIMBA KUIKOSA de AGOSTO YA ANGOLA