Home Sports WATATU WA SIMBA KUIKOSA de AGOSTO YA ANGOLA

WATATU WA SIMBA KUIKOSA de AGOSTO YA ANGOLA

MASTAA watatu wa Simba kesho wanatarajiwa kutokuwa sehemu ya msafara utakaolekea nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya de Agosto.

Alfajiri ya Jumamosi, kikosi cha Simba kinachonolewana Kocha Mkuu, Juma Mgunda kinatarajia kuanza safari kuelekea Angola kwa ndege ya kukodi.

Leo Ijumaa, Oktoba 7,2022 kikosi hicho kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye ardhi ya Dar kabla ya kukwea pipa.

Mgunda ameweka wazi kuwa wachezaji watatu watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti licha ya hali zao kuzidi kutengamaa.

“Mwanafamilia mwenzentu Shomari Kapombe yeye bado hajarejea kwenye ubora lakini anazidi kuimarika taratibu.

“Peter Banda na Jimsony Mwanuke hawa pia bado hawajawa imara, tunasikitika kuwakosa wachezaji hawa kwa kuwa ni familia yetu lakini hatuna namna.

“Uzuri ni kwamba wanaendelea vizuri ni jambo ambalo linafurahisha na tunapenda kuona kwamba wanarejea kwenye ubora ili kuendelea na kazi,” amesema.

Simba itaanzia ugenini Oktoba 9 kisha mchezo wa pili wa marudio utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Ilitinga hatua hiyo ya kimataifa kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Big Bullets ya Zambia.

Kiungo Pape Sakho ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia yeye amerejea na alikuwa sehemu ya wachezaji waliokuwa mazoezini leo Bunju.

Previous articleNABI: SISI HATUONGEI SANA NI KUTAFUTA MATOKEO
Next articleVIDEO: KIUNGO WA YANGA AWAITA MASHABIKI KWA MKAPA