Home Sports METACHA MNATA AWAPONZA SINGIDA BIG STARS

METACHA MNATA AWAPONZA SINGIDA BIG STARS

TIMU mbili Bongo zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zimekutana na rungu la kufungiwa kufanya usajili kwa dirisha moja kutokana na makosa ambayo wamefanya.

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 7,2022 na TFF, imeeleza namna hii:-“Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF), imezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine.

Uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa kuzingatia kanuni ya 47,(21) ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo. Adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili.

“Tanzania Prisons ilimsajili kipa Mussa Mbisa wa Coastal Union wakati ikifahamu kuwa ana mkataba na klabu hiyo nayo Singida Big Stars ilimsainisha mkataba kipa Metacha Mnata huku akiwa na mkataba na  Polisi Tanzania.

“Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imezikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni na ambazo zitakiuka kanuni zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni,” .

Ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na TFF.

Previous articleHII HAPA ORODHA YA MASTAA 25 WA AZAM FC KIMATAIFA
Next articleNABI: SISI HATUONGEI SANA NI KUTAFUTA MATOKEO