Home Sports VIUNGO WA KAZI YANGA WAANDALIWA KUIVAA AL HILAL

VIUNGO WA KAZI YANGA WAANDALIWA KUIVAA AL HILAL

VIUNGO wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda, Bernard Morrison, Jesus Moloko ni miongoni mwa nyota wanaondaliwa kwa ajili ya kuikabili Al Hilal ya Sudan.

Mbali na hao pia nyota wa kazi chafu Yannnick Bangala ambaye ni kiraka naye yupo kwenye mpango kazi wa mchezo ujao unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Oktoba 8,2022 Yanga itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Hatua ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo huo na wanaendelea na maandalizi.

“Nilifika mazoezini na niliona namna ambavyo benchi la ufundi linawapa maelekezo wachezaji na kila mmoja anakiu ya kupata ushindi.

“Unajua wanajua kwamba waandishi wanaandika kuhusu rekodi ya kushindwa kutinga hatua ya makundi kwa muda mrefu wao wanahitaji kufanya kweli kwa kupata matokeo, inawezekana na tupo tayari.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa,” .

Previous articleTIMU YA TAIFA YA WENYE ULEMAVU YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA
Next articleHESABU ZA SIMBA DAKIKA 180 KIMATAIFA