Home Sports HESABU ZA SIMBA DAKIKA 180 KIMATAIFA

HESABU ZA SIMBA DAKIKA 180 KIMATAIFA

 ANGA la kimataifa ndani ya dakika 180 litakutana na pumzi ya moto kutoka kwa vijana wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda baada ya kuweka wazi kuwa vijana wake wapo tayari.

Simba inatarajiwa kumenyana na de de Agosto na wataanzia ugenini Oktoba 9 nchini Angola kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 Mgunda amesema kuwa kazi ambayo wanafikiria kwa sasa ni mechi zao mbili za kimataifa namna watakavyopata matokeo.

“Unaona kwenye ligi mchezo wetu dhidi ya Dodoma umekwisha matokeo huwezi kuyabadili ambacho kinakwenda kufanyiwa kazi ni makosa na malengo ni kuona tunashinda kwenye mechi zetu za kimataifa.

“Huwezi kusema kwamba hakuna asiyependa kuona timu inapata matokeo hakuna na tunajua kwamba ushindani ni mkubwa , ukweli ni kwamba tupo tayari na tutapambana kufanya vizuri,” alisema Mgunda.

Previous articleVIUNGO WA KAZI YANGA WAANDALIWA KUIVAA AL HILAL
Next articleVIDEO:KWA MARA YA KWANZA PRIVA AKIWA YANGA UCHAMBUZI WAKE