Home Uncategorized TIMU YA TAIFA YA WENYE ULEMAVU YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA

TIMU YA TAIFA YA WENYE ULEMAVU YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA

TIMU ya Taifa ya Watu wenye ulemavu Tanzania (Tembo Warriors,) imefuzu kuingia katika hatua 16 bora katika mashindano ya kombe la dunia la mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu.

Tanzania ilipata ushindi wake wa kwanza wakiifunga Uzbekistan mabao 2-0 huko Uturuki yanapoanyika mashindano hayo.

Tembo Warriors sasa watakutana na Japan katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa leo Oktoba 5,2022.

Tanzania ilikua kundi E pamoja na Spain, Poland na Uzbekistan

Nchi nyingine zilizofuzu katika nafasi hiyo kutoka Afrika ni Morroco na Angola.

Mashindano haya yameanndaliwa na Shirikisho la Soka la Duniani (WAFF), na yanafanyika Istanbul, Uturuki hadi 9 Oktoba 2022.

Previous articleYANGA YAMTEKA BOSI WA AL HILAL, SIMBA KUWAFUATA WAANGOLA KITEMI
Next articleVIUNGO WA KAZI YANGA WAANDALIWA KUIVAA AL HILAL