Home Sports MZAMIRU YASSIN AINGIA KWENYE VITA MATATA SIMBA

MZAMIRU YASSIN AINGIA KWENYE VITA MATATA SIMBA

MASTAA watatu wa kikosi cha Simba wameingia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Septemba.

Nyota hao wanawania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) ambapo mshindi huchaguliwa na mashabiki.

Ni mshambuliaji Moses Phiri na kiungo Clatous Chama hawa wote ni raia wa Zambia pamoja na mzawa Mzamiru Yassin.

Mzawa Mzamiru anaingia kwenye vita ngumu kuwania tuzo hiyo akiwa mzawa pekee aliyepenya kwenye tatu bora.

Kwa mwezi Agosti walipenya viungo watatu kwenye tuzo hiyo ambao ni Chama raia wa Zambia, Sadio Kanoute raia wa Mali na Pape Sakho raia wa Senegal.

Ni Chama alisepa na tuzo hiyo ambapo kwa mwezi Agosti alifanikiwa kufunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Previous articleNABI AWAPA MAAGIZO WACHEZAJI WAKE
Next articleMRITHI WA SENZO YANGA ATAMBULISHWA