Home Sports NABI AWAPA MAAGIZO WACHEZAJI WAKE

NABI AWAPA MAAGIZO WACHEZAJI WAKE

KWENYE Ligi Kuu Bara, ukuta wa Yanga unaoongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto umeruhusu mabao matatu ya kufungwa huku safu ile ya ushambuliaji ikiwa imetupia jumla ya mabao 9.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hila unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni Oktoba 8,2022 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ambapo timu zote zinahitaji kupata ushindi ili kutinga hatua ya makundi.

Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amesema kuwa ni muhimu kwa safu ya ulinzi kuongeza umakini ili kupunguza makosa.

“Muhimu kwa safu ya ulinzi kuwa makini na kuongeza hali ya kupunguza makosa hilo litafanya tusifungwe mabao mengi.

“Jambo la msingi ni kuona kwamba tunashinda mechi ambazo tunashinda, kila kitu kinawezekana na nina amini kwamba inawezekana kushinda,”.

Kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele kafunga mabao matatu kwenye nne ambazo Yanga imecheza msimu wa 2022/23.

Kwenye mechi mbili za kimataifa dhidi ya Zalan FC, Yanga haikufungwa zaidi ya kufunga mabao 9 yaliyowapa nafasi ya kusonga mbele hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Previous articleDE GEA KAINGIA ANGA ZA JUVENTUS
Next articleMZAMIRU YASSIN AINGIA KWENYE VITA MATATA SIMBA