Home Uncategorized MRITHI WA SENZO YANGA ATAMBULISHWA

MRITHI WA SENZO YANGA ATAMBULISHWA

UONGOZI wa Yanga leo Septemba 27,2022 umemtangaza Adre Mtine kutoka Zambia kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu hiyo.

Ni mkataba wa miaka miwili CEO huyo amepewa kufanya kazi ndani ya Yanga ambapo utambulisho wake umefanywa na Rais wa Yanga, Injinia Hers Said.

Anakuja kuchukua mikoba ya Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini ambaye mkataba wake ulipogota ukingoni hakuwa tayari kuongeza.

Taarifa iliyotolewa na Yanga hivi karibuni kuhusu Mbatha ni kwamba licha ya kufanya mazungumzo ya kuhitaji kuona akiongeza dili jipya kwa mara nyingine aligomea kwa kueleza kuwa anahitaji kuwa karibu na familia yake.

Injinia ameweka wazi kuwa malengo ya kufanya naye kazi ni kuona kwamba Yanga inafikia mafanikio makubwa ambayo wameweka.

Nafasi hiyo kwa muda ilikuwa chini ya Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick.

Previous articleMZAMIRU YASSIN AINGIA KWENYE VITA MATATA SIMBA
Next articleMERIDIANBET WAISHIKA MKONO HOSPITALI YA MADALE KWA KUWAPA VIFAA