Home Uncategorized KANE AKUBALI KASI YA HAALAND

KANE AKUBALI KASI YA HAALAND

 MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Harry Kane raia wa England ameweka wazi kuwa kasi ambayo ameanza nayo mshambuliaji mpya ndani ya Manchester City, Erling Haaland ni nzuri ila naye ataongeza juhudi kutimiza majukumu yake.

Haaland raia wa Norway amekuwa chachu ya matokeo mazuri uwanjani ametupia jumla ya mabao 14 kwenye mechi za mashindano yote.

Ni namba moja kwa watupiaji ndani ya Ligi Kuu England akiwa ametupia mabao 11 kwenye mechi saba.

Kane mwenye miaka 29 naye ameanza msimu kwa umakini akiwa ametupia mabao sita kwenye mechi saba za ligi.

“Kila mtu anazungumza kuhusu Haaland kwa kuwa amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu. Kama mnavyonijua mimi huwa sijikiti sana kwenye kuangalia sana watu wengine hapana ninajiangalia mimi mwenyewe na kile ninachoeweza kukifanya,” amesema.

Previous articleSIMBA ILEE MAKUNDI CAF, NABI AWAONGEZEA PROGRAM MAYELE,KISINDA
Next articleVIDEO:MSIKIE TWAHA KIDUKU BAADA YA KUMPA KICHAPO MWARABU