Home Sports YANGA WAIPIGIA HESABU AL HILAL

YANGA WAIPIGIA HESABU AL HILAL

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wameona ubora wa wapinzani wao Al Hilal ya Sudan hivyo watafanya maandalizi mazuri kupata matokeo.

Nabi amesema ameona ubora wa Al Hilal ambao ameuficha kwa kukataa kuuweka wazi kwa kuhofia wapinzani kushtuka, zaidi akipanga kukiimarisha zaidi kikosi chake ili kuhakikisha anapata ushindi nyumbani na ugenini.

“Mimi ni kama mwanajeshi, muda wowote nipo tayari kwa ajili ya mapambano, hivyo kukutana na Al Hilal nilitarajia.

“Hivyo kama kocha nimekuwa na utaratibu wa kuwafuatilia wapinzani wangu kwa kuziangalia video za michezo yao ya mwisho waliyocheza kwa ajili ya kuwajua zaidi.

“Wapinzani wetu Al Hilal tayari nimewaona na kuwafahamu wachezaji hatari wa kuchungwa, mbinu na mfumo wanaoutumia, kikubwa ninaendelea kukinoa kikosi changu kitakachopata ushindi,” alisema Nabi.

Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya Al Hilal ambapo mechi ya kwanza inatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 8, kisha marudiano ni Sudan kati ya Oktoba 14 na 16, mwaka huu.

Previous articleKOCHA MBRAZILI AIBUKIA SIMBA, MASTAA YANGA WAIAPIA AL HILAL
Next articleWINGA DEMBELE ASIMULIA ALIVYOPOTEZA MIAKA MITANO