Home Sports LUSAJO NEMBO YA MABAO UWANJANI

LUSAJO NEMBO YA MABAO UWANJANI

NEMBO ya Relliats Lusajo ukifika Uwanja wa Mkapa utaiona juu ikiwa metulia, fahari kubwa kwa anachokifanya ni jambo la kujivunia kwa mzawa huyu.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 alianza kwa kasi ya namna hii kwenye kucheza na nyavu mwisho akagotea namba 10.

Pia alikuwa ni namba moja kwenye kutengeneza mabao alitengeneza pasi 6 za mabao hakika miguu yake ina ushkaji na nyavu.

Kwa msimu huu ni namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi akiwa ametupia mabao matano katika mechi tano mfululizo.

Hajapoa kwenye mechi zote ambazo ameanza alikuwa anafunga na anatimiza majukumu yake bila kuogopa.

Anastahili pongezi na kuongeza juhudi kutimiza malengo yake pamoja na malengo ya timu ili aweze kuvunja rekodi yake mwenyewe.

Huyu hapa Lusajo anazungumzia kasi yake hiyo:”Kikubwa ni ushindi kwa ajili ya timu na inapata matokeo, ushindani ni mkubwa na sisi tunazidi kupambana,”.

Kwenye mabao matano ambayo amefunga ni bao moja kafunga kwa mkwaju wa penalti mbele ya Coastal Union huku akiifunga Mtibwa Sugar mabao mawili.

Previous articleKOCHA TAIFA STARS ABEBA MATUMAINI KIMATAIFA
Next articleRUVU SHOOTING: TUMEJIPANGA KUFANYA VIZURI