Home Sports KOCHA TAIFA STARS ABEBA MATUMAINI KIMATAIFA

KOCHA TAIFA STARS ABEBA MATUMAINI KIMATAIFA

HONOUR Janza, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wtacheza kwa kujiamini kwenye mechi za kirafiki za kimataifa zilizo kwenye Kalenda ya FIFA ili kupata matokeo.

Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uganda na Libya ambazo zitachezwa nchini Libya na kikosi hicho kilikwea pipa jana, Septemba 20 kuelekea Libya.

Katika msafara huo miongoni mwa nyota ambao walikuwa katika kikosi hicho ni pamoja na Said Ndemla kiungo anayekipiga Singida Big Stars ambaye aliongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa Stars, Himi Mao,Dickson Job,Aishi Manula ni miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye msafara huo.

 Kocha huyo amesema:”Tunaamini mechi hizi za kimataifa za kirafiki zitazidi kutuimarisha na tutafanya kazi kubwa kwa kucheza kwa kujiamini ili kupata ushindi, wachezaji wapo tayari na tunaamini tutafanya vizuri,” .

Stars imewasili salama nchini Libya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mechi hizo mbili.

Tanzania itaanza kucheza na timu ya Taifa ya Uganda Septemba 24 na mchezo wa pili dhidi ya Libya unatarajiwa kuchezwa Septemba 27.

Previous articleTHE PIRATES, NDANI YA MERIDIANBET: FURAHIA SLOTI HII YA PIRATES POWER!
Next articleLUSAJO NEMBO YA MABAO UWANJANI