Home Sports RUVU SHOOTING: TUMEJIPANGA KUFANYA VIZURI

RUVU SHOOTING: TUMEJIPANGA KUFANYA VIZURI

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting ameweka wazi kuwa msimu huu wamejipanga kufanya vizuri kwenye mechi zao zote watakazoshuka uwanjani.

Bwire ameongeza kuwa msimu huu ni tofauti na uliopita jambo linawapa nguvu ya kuongeza juhudi ili kuleta ushindani.

“Msimu huu ni watofauti na kila timu inahitaji ushindi nasi tupo tayari ukizingatia kwamba tumefanya usajili mzuri.

“Benchi la ufundi nalo lina mbinu zake katika kutafuta ushindi, mashabiki wawe pamoja nasi tupo imara na tutafanya vizuri,” amesema.

Mchezo wao wa ufunguzi Ruvu Shooting ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu wakiwa ugenini na mchezo wa pili walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo wao uliopita walishinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Previous articleLUSAJO NEMBO YA MABAO UWANJANI
Next articleSAUTI: MABOSI SIMBA WAMJADILI KOCHA MPYA