Home Sports SIMBA YASONGA MBELE KIMATAIFA, PHIRI KAWA MCHARO

SIMBA YASONGA MBELE KIMATAIFA, PHIRI KAWA MCHARO

KATIKA mabao manne ambayo Simba imefunga kimataifa matatu yamefungwa na Moses Phiri ambaye kafunga mechi zote mbili hatua ya awali mfululizo.

Mchezo wa awali uliochezwa nchini Malawi dhidi ya Big Bullets Phiri alitupia bao moja na lingine ni mali ya mzawa John Bocco.

Leo Septemba 18,2022 wakati Simba ikishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Big Bullets tena ni mabao ya Phiri ambaye alifunga lile la kuongoza dakika ya 28 na lile la pili dakika ya 50.

Simba inasonga hatua inayofuata kimataifa kwa jumla ya mabao 4-0 ambapo kipa Aishi Manula ndani ya dakika 180 hajaokota bao kwenye lango lake.

Shukran kwa mzawa Israel Mwenda ambaye anazidi kuwa imara kila akipewa majukumu ana kazi ya kuongeza juhudi na kujiamini ili awe bora zaidi.

Kiungo Pape Sakho ambaye alianzia benchi hakuweza kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa.

Juma Mgunda , Kocha Mkuu wa Simba amesema furaha kwa ushindi ni kwa kila mmoja ambaye amejitokeza leo kuipa sapoti Simba.

Previous articleRB LEIPZIG YAPIGWA 3-0 BUNDESLIGA
Next articleVIDEO: HUYU HAPA KOCHA WA BIG BULLETS AKUBALI UKUBWA WA SIMBA