Home Sports WINGA WA SPIDI KISINDA KUKIWASHA YANGA

WINGA WA SPIDI KISINDA KUKIWASHA YANGA

NYOTA Tuisila Kisinda anarejea rasmi kuongeza kasi ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, hivyo anatarajiwa kukiwasha ndani ya ligi na kimataifa.

Usajili wakeakitokea RS Berkane ulileta mvutano mkubwa ila rasmi Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Mpira Tanzania, (TFF) imepitisha usajili wake.

Usajili wa winga huyo umekamilika baada ya Yanga kumtoa mshambuliaji Lazarous Kambole na nafasi yake kuchukuliwa na Kisinda ili kutimiza idadi ya wachezji 12.

Ikumbukwe kwamba awali TFF ilitoa taarifa iliyoeleza kuzuia usajili wa wachezaji wengine kwa kuwa idadi ilikuwa imekamilika na dirisha lilikuwa limefungwa

“Awali kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wakigeni.

“Licha ya Changamoto hiyo pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa, (ITC) ambayo tayari imeshapatikana.

“HIvyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma kwa mujibu wa kanuni ya 62, (1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

“Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu Uganda na tayari TFF imetoa ITC,” ilieleza taarifa hiyo.

Previous articleSIMBA HESABU ZAO NI KWA BIG BULLETS
Next articleVIDEO: CHEKI MASTAA SIMBA WALIVYOREJEA DAR