Home Sports MASTAA SIMBA WAPEWA ANGALIZO KIMATAIFA

MASTAA SIMBA WAPEWA ANGALIZO KIMATAIFA

CLATOUS Chama, kiungo wa Simba pamoja na wachezaji wengine ikiwa ni nahodha John Bocco, Moses Phiri na Aishi Manula wamepewa angalizo kuelekea mchezo wao dhidi ya Nyasa Big Bullets wa marudio.

Simba inatarajiwa kumenyana na Big Bullets Jumapili ikiwa inakumbuka imetoka kushinda mabao 2-0 ugenini na mabao yakifungwa na Phiri pamoja na Bocco.

Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa baada ya mchezo huo walifanya kikao na wachezaji.

“Tulimaliza mchezo wetu dhidi ya Nyasa Big Bullets tumewaambia wachezaji kuwa mechi bado haijaisha na wachezaji wanapaswa kufanya vizuri kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa marudio.

“Kumbukumbu ya Jwaneng Galaxy kututoa kwenye mchezo wetu Uwanja wa Mkapa baada ya ule wa awali kushinda mabao 2-0 ulitupa somo hatutakubali kuona hili linajirudia.

“Walikuwepo wachezaji wetu John Bocco, Aishi Manula, Beno Kakolanya, wote walikuwepo kwenye mchezo ambacho tumeongea nao ni kwamba lazima tuchulue tahadhari kwa mchezo wetu ujao ili kusonga mbele kimataifa,” amesema Ally.

Previous articleCR 7, SANCHO WAWAPA FURAHA MASHABIKI UNITED
Next articleSAUTI:MOSES PHIRI AMTANGAZIA VITA MAYELE