Home Sports KOCHA SINGIDA BIG STARS AWAPA MBINU WACHEZAJI

KOCHA SINGIDA BIG STARS AWAPA MBINU WACHEZAJI

MATHIAS Lule, Kocha Msaidizi wa Singida Big Stars amesema kuwa wachezaji wote ambao wapo ndani ya kikosi hicho watapata nafasi ya kucheza.

Singida Big Stars kwa sasa inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Septemba 21.

Miongoni mwa mastaa ambao wapo ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Amis Tambwe, Meddie Kagere, Aziz Andambwile, Pascal Wawa ambaye ni nahodha wa kikosi hicho.

“Hakuna mchezaji ambaye anapenda kuanza benchi lakini hilo lipo kwenye maamuzi ya benchi hivyo wale wanaopata nafasi wanacheza kwa kushirikiana na wale ambao wataanza.

“Ni suala la muda tu kila mchezaji atapata nafasi ya kucheza kwani kila aliyepo hapa anastahili kucheza ndio maana akasajiliwa kikubwa kwao ni kuonyesha jitihada,” amesema.

Kwenye msimamo Singida Big Stars imekusanya pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu ikiwa nafasi ya tano.

Previous articleYANGA INAUZA ULAYA,BIG BULLETS YAHOFIA MUZIKI WA SIMBA
Next articleSIMBA HESABU ZAO NI KWA BIG BULLETS