Home Sports YANGA YAICHAPA MTIBWA 3-0, AZIZ KI ATUPIA

YANGA YAICHAPA MTIBWA 3-0, AZIZ KI ATUPIA

WAKATI Yanga ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ni mabao ya Djuma Shaban dakika ya 32, Fiston Mayele dakika ya 37 na Aziz KI dakika ya 90 yalitosha kuipa pointi tatu Yanga inayofikisha pointi 10 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wachezaji walicheza kwa umakini kipindi cha kwanza na walitumia nafasi ambazo walizipata.

Kipa Diara Djigui alikuwa langoni leo baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita wa kimataifa dhidi ya Zalan FC kwa kuwa alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Ni bao la kwanza kwa Aziz KI kwenye ligi ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 ambapo aliibuka hapo akitokea kikosi cha ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Faroukh Shikalo kipa wa Mtibwa Sugar raia wa Kenya hakuwa na chaguo leo kwa kuwa jitihada zake kuokoa michomo zilikwama.

Previous articleKIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOINGIA KAMBINI KUIKABLI LIBYA
Next articleONYANGO NDANI YA SIMBA, KAZI INAANZA MBEYA