Home Sports ONYANGO NDANI YA SIMBA, KAZI INAANZA MBEYA

ONYANGO NDANI YA SIMBA, KAZI INAANZA MBEYA

BEKI wa kati wa Simba, Joash Onyango ni miongoni mwa nyota wa kikosi hicho ambao wamewasili salama Mbeya, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons unaotarajiwa kuchezwa kesho, Septemba 14, Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Wengine ni pamoja na Aishi Manula ambaye leo ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Henock Inonga.

Kwa upande wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu, Juma Mgunda na msaidizi wake Seleman Matola wapo kwenye msafara huo uliopo Mbeya, ‘Green City’.

Ikumbukwe kwamba Onyango alikuwa kwenye mvutano na mabosi wake hao kushusu mkataba wake ambapo alikuwa anaomba asepe lakini kutokana na mambo kwenda sawa bado yupoyupo Msimbazi.

Onyango hakuwa sehemu ya kikosi kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara zama za Zoran Maki ambaye anatajwa kuwa alikuwa hana uhitaji wa kumtumia beki huyo.

Ahmed Ally, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa beki huyo ni mali ya Simba kwa kuwa ana mkataba wa miaka miwili.

“Onyango ana mkataba na Simba na aliongeza mkataba wa miaka miwili hivyo bado yupo kwenye kikosi na ataendelea kuhudumu katika kikosi chetu,” .

Previous articleYANGA YAICHAPA MTIBWA 3-0, AZIZ KI ATUPIA
Next articleVIDEO: WALICHOKIFANYA YANGA BAADA YA USHINDI MBELE YA MTIBWA