Home Sports KAZI KIMATAIFA BADO NI NGUMU

KAZI KIMATAIFA BADO NI NGUMU

MECHI za awali zimeanza kwenye mechi za kimataifa na tunaona wawakilishi wa Tanzania wameanza kupata matokeo chanya katika mechi za awali.

Pia zipo ambazo zimepata matokeo ambayo walikuwa hawayahitaji wala kuyatarajia ni muhimu kupanga mipango upya kwa ajili ya mechi zijazo.

Kila hatua ambayo inapigwa ni muhimu kufanya maandalizi mazuri kwa kuwa hakuna matokeo yanayopatikana kwa kufikiria bila utendaji wa kazi uwanjani.

Hapa tunaona kwamba wawakilishi kwenye mechi za kimataifa kila mmoja anapeperusha bendera ya Tanzania akiwa na malengo ya kupata matokeo mazuri.

Inawezekana lakini kama hakutakuwana mipango makini baada ya kumaliza mchezo mmoja kutakuwa na matokeo mengine tofauti na vile ambavyo mashabiki na uongozi wa timu husika unahitaji.

Kwa namna ambavyo timu itakuwa imeweza kufanya maandalizi yake itakuwa kwenye namna yake ya kupata matokeo.

Kwa kilichopatikana kwenye mechi za wakati huu ni mpango kazi uliopangwa wakati uliopita kwa kazi iliyokuwa inafanywa kwenye uwanja wa mazoezi.

Msimu mpya kimataifa ni wakati mpya wa kufanya mambo mengine tofauti na wakati uliopita hiyo itawafanya kila mmoja apate matokeo chanya.

Ipo wazi kwamba maisha yakwenye mechi za kimataifa yana utofauti mkubwa na maisha ya ligi hasa kwenye upande wa mashindano husika na aina ya mechi ambazo zinachezwa kuwa na ushindani mkubwa.

Wachezaji kazi yao ni moja kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ili waweze kupata kile wanachokistahili,kikubwa ni mipango kazi na ushirikiano.

Ni wakati mzuri wa kujipanga tena na timu kuangalia yale ambayo waliweza kuyafanya msimu uliopita na kushindwa kufikia malengo ambayo walikuwa wamejiwekea kitaifa na kimataifa.

Kupata matokeo kwenye mechi za awali ni hatua kubwa na itazidi kuongeza hali ya kujiamini kwa timu husika kwenye kutafuta matokeo uwanjani.

Tanzania inakwenda kupeperushwa na timu nne ambazo nina amini zote zina uwezo mkubwa na visiwani Zanzibar pia kuna timu mbili ambazo zinapeperusha bendera muhimu timu zote zikawa na matokeo chanya.

Fursa nyingine kwa wachezaji kuwa sokoni kwenye anga la kimataifa hili ni jambo kubwa ambalo litawafanya wazidi kuimarika na kuwa na thamani zaidi sokoni kitaifa na kimataifa.

Ipo wazi kwamba mashindano ya kimataifa yanahitaji maandalizi mazuri ili kuweza kupata matokeo chanya kwenye kila mechi.

Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba kwenye mashindano ya kimataifa kwa mara nyingine tena kuona kila mmoja anashindwa kusonga mbele.

Wapinzani nao wanatambua kinachohitajika ni matokeoya ushindi iwe mechi inachezwa ugenini ama nyumbani inawezekana kushinda.

Nina amini kwamba wachezaji ambao walishawahi kushiriki mashindano ya kimataifa wanaona  namna wanavyozidi kupata uzoefu kwenye kila hatua na hili ni jambo zuri.

Kadri ambavyo wanaata nafasi ya kucheza kimataifa wanangeza hali ya uzoefu kwa wale wazawa inakuwa kazi nyingine ya kuongeza hali ya kujiamini pale watakapoitwa timu ya taifa ya Tanzania kutimiza majukumu mengine.

Jambo la muhimu ni maandalizi mazuri kwa mechi na kupata matokeo, wachezaji jitoeni bila kuogopa kwa ajili ya kupambania timu na kutimiza majukumu yenu.

Previous articleVIDEO:TAZAMA MASTAA SIMBA WALIVYOTUA DAR
Next articleVIDEO: JUMA MGUNDA AFUNGUKIA ISHU YA VYETI