Home International YANGA WACHAPA 4G KIMATAIFA

YANGA WACHAPA 4G KIMATAIFA

UBAO wa Uwanja wa Mkapa umesoma Zalan 0-4 Yanga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa kipindi cha pili baada ya dakika 45 ubao kusoma Zalan 0-0 Yanga.

Fiston Mayele ambaye katupia mabao matatu mwenyewe alianza kufunga bao la kuongoza dakika ya 47 na mengine mawili alifunga dakika ya 84 na 87.

Shukrani kwa mzawa Feisal Salum ambaye alifunga bao moja kwenye mchezo huo dakika ya 51 na kuwafanya Yanga kuibuka na ushindi huo wakiwa ugenini.

Mchezo ujao kwa Yanga wa marudio watakuwa nyumbani ambapo unatarajiwa kuchezwa Septemba 17, Uwanja wa Mkapa.

Yanga ina faida ya mabao manne ya ugenini hivyo kazi yao ni kushinda mchezo ujao ili kuongeza nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Previous articleBIG BULLETS 0-1 SIMBA, LIGI YA MABINGWA
Next articleSIMBA YAANZA KWA USHINDI KIMATAIFA