Home Sports SPORTPESA YACHANGIA SACCOS YA AKINA MAMA KIZIMKAZI

SPORTPESA YACHANGIA SACCOS YA AKINA MAMA KIZIMKAZI

KAMPUNI ya michezo ya burudani na ubashiri Sportpesa wikiendi imeshiriki Tamasha
maalum la kizimkazi na kuchangia mfuko wa Saccoss ya kina mama kwa ajili ya
kuboresha hali zao za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa tamasha, baada ya kupewa nafasi ya kutoa neno la
shukrani, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Sportpesa Tarimba Abbas,
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa
mwaliko na pia kwa nafasi ya ushiriki.

‘’Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunialika mimi binafsi na kwa
upande mwingine kampuni yetu ya Sportpesa, na pia kwa kunipa nafasi ya kutoa
neno la shukrani kwa wananchi wa eneo hili.

“Kampuni ya Sportpesa ilivutiwa na wazo la
kushiriki kuchangia ama kuongeza mtaji kwenye Saccoss ya akina mama, ambapo
kupitia saccoss hiyo akina mama watapata fursa ya kupata mikopo midogo midogo
itakayowasaidia katika kuboresha hali zao.

“Kwa kuanzia Kampuni yetu ya Sportpesa tayari imeshatia fedha katika Saccoss
hiyo ya akina mama na nisingependa kutaja kiasi ila tambueni ni fedha nyingi. Na pia
mwakani pia tutaweka tena fedha zingine ili iwe chachu ya kuleta
maendeleo kwa akina mama’’. Amesema Tarimba.

Pia Tarimba amemshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo amepeleka
maendeleo katika jimbo la Kizimkazi ambapo kwa yeyote ambaye ameshabahatika
kufika miaka kadhaa iliyopita ataona tofauti baina ya siku za nyuma na sasa.

‘’’Napenda kukupa pongezi kwa namna ulivyowaletea maendeleo wananchi wa
maeneo haya kwani kwa sisi ambao tumebahatika kufika hapa mara kwa mara
tunaona tofauati.

Kwa mara ya kwanza SportPesa ilishiriki kwa kukarabati nyumba ya madaktari wawili
ambazo zinatoshelezea familia mbili ili kuhakikisha urahisi wa wanakizimkazi kupata
huduma pale inapohitajika.

Kama ilivyo nia ya SportPesa kuendeleza na kukuza mpira wa miguu nchini
tuliendea kudhamini timu ndogo ndogo za mpira wa miguu kwa kuwapatia vifaa vya
michezo ikiwemo jezi.

Previous articleFEI TOTO ACHEKELEA KUTUPIA MABAO YA MBALI
Next articleKOCHA MPYA SIMBA KUANZA NA WAMALAWI KIMATAIFA