Home Sports KOCHA MPYA SIMBA KUANZA NA WAMALAWI KIMATAIFA

KOCHA MPYA SIMBA KUANZA NA WAMALAWI KIMATAIFA

 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini watafanya vizuri kwenye mechi yao dhidi ya Big Bullets inayotarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi nchini Malawi ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mgunda amekabidhiwa mikoba kwa muda ndani ya Simba ambayo kwa sasa inatafuta kocha mpya baada ya kuachana na Zoran Maki aliyechukua mikoba ya Pablo Franco.

Kazi yake ya kwanza ni Septemba 10,2022 na tayari ameanza kuwafundisha wachezaji wa Simba ikiwa ni pamoja na Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, John Bocco na Clatous Chama.

Mgunda amesema:”Ni mapema sana kuanza kuzungumzia kile ambacho ninaweza kufanya kwa muda huu mchache ambao nimepewa kuiongoza Simba.

“Lakini tunajua kwamba Simba ni timu kubwa na inashiriki mashindano makubwa hususani haya ya kimataifa hivyo tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema.

Previous articleSPORTPESA YACHANGIA SACCOS YA AKINA MAMA KIZIMKAZI
Next articleVIDEO:MECHI YA YANGA V AZAM FC KULIKUWA NA KADI NYEKUNDU