Ni Feisal Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC anaongoza chati kwenye ufungaji msimu wa 2025/26 ndani ya ligi namba 6 kwa ubora Afrika.
Kiungo huyo anaongoza chati kwenye ufungaji akiwa na magoli 14 anafuatiwa na kiungo wa Yanga SC, Allen Okello mwenye magoli 11.
Mshambuliaji namba moja kwenye chati ya ufungaji ni Prince Dube naye ni mali ya Yanga SC akiwa amefunga jumla ya magoli 9. Ni mzunguko wa pili sasa timu zimebakiza mechi 5.
Mei 25, 2026 wakati wakipata ushindi wa magoli 3-0 KMC FC, Uwanja wa Azam Complex kiungo huyo alifunga magoli mawili na kuchaguliwa kuwa Man of the Match.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.