Home International DIEGO COSTA APATA KIBALI CHA KAZI KUIBUKIA WOLVES

DIEGO COSTA APATA KIBALI CHA KAZI KUIBUKIA WOLVES

MSHAMBULIAJI mkongwe, Diego Costa mwenye miaka 33 anatarajiwa kusaini mkataba mfupi wa mwaka mmoja na Klabu ya Wolves baada ya kupata kibali cha kufanya kazi tena England.

Raia huyo wa Hispania aliicheza Chelsea kuanzia 2014-17 alipigiwa simu na Wolves baada ya mshambuliaji wao waliyemnunua katika dirisha hili, Sasa Kalajdzic kuumia goti huku Paul Jimenez akiwa ni majeruhi.

Nyota huyo kwa sasa hana timu baada ya kuondoka Atletico Mineiro ya Brazil, Januari hivyo ameruhusiwa kusajiliwa kama mchezaji huru hata kama dirisha limefungwa.

Awali kibali cha Costa kilikataliwa lakini Wolves wakakata rufaa na juzi Jumatano akapata kibali hicho hivyo anakwenda kuanza changamoto mpya.

Previous articleVIDEO:MECHI YA YANGA V AZAM FC KULIKUWA NA KADI NYEKUNDU
Next articleVIDEO:JEMBE AZUNGUMZIA SAKATA LA KISINDA NA MGUNDA KUINOA SIMBA