Home Sports KOCHA MTIBWA ATAJA SABABU ZA KUPOTEZA MECHI TATU

KOCHA MTIBWA ATAJA SABABU ZA KUPOTEZA MECHI TATU

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa makosa ambayeo wameyafanya kwenye mechi tatu mfululizo yamewafanya waadhibiwe kwa kufungwa.

Katwila amebainisha kwamba jambo ambalo halikuwa kwenye mpango waoni kupoteza mechi na hakuna mchezaji walakiongozi ambaye anapenda iwe hivyo.

“Imetokea tumepoteza kwenye mechi zetu tatu hili ni jambo baya na hakuna ambaye anapenda kuona inakuwa hivyo ni matokeo.

“Tumefanya makosa kwenye mchezo wa kwanza tukayarekebisha yakaja yakatokea makosa mengine tukarekebisha tena tukakosea hili tutalifanyia kazi kwa kuwa kupoteza sio jambo zuri,” amesema.

 Ihefu ilianza kwa kupoteza kwa kufungwa dhidi ya Ruvu Shooting kisha ikapoteza mbele ya Namungo ilikuwa nyumbani kwa kufungwa bao mojamoja na timu hizo.

 Kwenye mchezo wa tatu imefungwa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ilikuwa ugenini mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu,Morogoro.

Previous articleMABOSI SIMBA WAVUTANA KISA KOCHA MPYA,MKATABA WAMBANA BM
Next articleSIMBA WAKWEA PIPA KUELEKEA MALAWI