Home Sports SIMBA WAKWEA PIPA KUELEKEA MALAWI

SIMBA WAKWEA PIPA KUELEKEA MALAWI

KIKOSI cha Simba ambacho kipo chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda leo Septemba 8 kimeanza safari kuelekea nchini Malawi.

Safari hiyo ni kwa ajili ya kuelekea kufanya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Big Bullets ya Malawi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 10,2022 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 18,2022.

Mgunda amekabidhiwa mikoba ya Zoran Maki ambaye alifikia makualiano ya kuvunja mkataba na timu hiyo aada ya kuiongoza kwenye mechi mbili za ligi akishinda zote mbele ya Kagera Sugar na Geita Gold.

Atafanya kazi kwa kushirikiana na Matola ambao wote ni wazawa na waliwahi kufanya kazi pamoja kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa nyakati tofauti.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na kiungo Clatous Chama, Pape Sakho, Henock Inonga na Sadio Kanoute.

Previous articleKOCHA MTIBWA ATAJA SABABU ZA KUPOTEZA MECHI TATU
Next articleFEI TOTO ACHEKELEA KUTUPIA MABAO YA MBALI