Home Sports NAMUNGO YASHINDA MBELE YA IHEFU, LUSAJO KAMA KAWA

NAMUNGO YASHINDA MBELE YA IHEFU, LUSAJO KAMA KAWA

MCHEZO pekee wa Ligi Kuu Bara ambao umechezwa leo Agosti 19,2022 Uwanja wa Uhuru dakika 90 ubao umeseoma Ihefu 0-1 Namungo FC.

Huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa timu ya Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila kupoteza pointi tatu ikiwa nyumbani.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Highland Estate, Ihefu ilifungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Ally Bilal dk ya 18 akiwa ndani ya 18 akitumia mguu wa kushoto.

Leo bao la Namungo FC limepachikwa na nahodha Relliats Lusajo ambaye jina lake pia limetajwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini Agosti 21 kwa maandalizi ya CHAN dhidi ya Uganda.

Dakika 45 ngoma ilikuwa nzito kwa timu zote mbili na bao lilipatikana kipindi cha pili dakika ya 50 ambapo Lusajo akiwa mbele ya mabeki wa Ihefu ambao walishindwa kumzuia nyota huyo aliweza kufunga.

Inakuwa ni bao la tatu la Lusajo kwa msimu wa 2022/23 kwa kuwa mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar alifunga mabao mawili wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Namungo 2-2 Mtibwa Sugar.

Lusajo amesema: “Furaha yetu ni kuona tunapata matokeo na kufuata maelekezo ambayo tumepata haikuwa mechi rahisi lakini tumeshinda,”.

Previous articleVIDEO:JONAS MKUDE,MANULA,JOB,LUSAJO NDANI YA TAIFA STARS
Next articleNABI KUIKABILI COASTAL UNION, AKIRI KUTUMIA NGUVU KWA POLISI