Home Sports NABI KUIKABILI COASTAL UNION, AKIRI KUTUMIA NGUVU KWA POLISI

NABI KUIKABILI COASTAL UNION, AKIRI KUTUMIA NGUVU KWA POLISI

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema walitumia nguvu nyingi kwenye msako wa pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania hivyo wanajipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa ni wa pili kwa Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi utachezwa kesho Agosti 20, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imetoka kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheik Amri Abeid, Agosti 17,2022.

Nabi amesema: “Tumetumia nguvu nyingi mchezo wetu uliopita dhidi ya Polisi Tanzania lakini ambacho tumekipata ni ushindi tumefurahi tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu ujao.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu, wachezaji wapo tayari kuweza kutafuta ushindi ili kuweza kuendelea pale ambapo tuliweza kuishia,” amesema.

Previous articleNAMUNGO YASHINDA MBELE YA IHEFU, LUSAJO KAMA KAWA
Next articleSAUTI:SIMBA WAUKUBALI MUZIKI WA YANGA