Home Sports SIMBA QUEENS YAPATA USHINDI KIMATAIFA

SIMBA QUEENS YAPATA USHINDI KIMATAIFA

SIMBA Queens leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Corporate FC kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kwa Wanawake uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ni wakuwania kupata nafasi ya kufuzu mashindano hayo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa dk zote 90.

Mabao ya Simba yamefungwa na Aquino Corazone dk ya 21 akitumia pasi ya Bukulu aliyepiga faulo  na Pambani Kuzoya alipachika bao dk ya 61.

Simba wameanza kwa ushindi wakiwa nyumbani jambo ambalo linawapa nguvu ya kuweza kusonga mbele hatua inayofuata.

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA DHIDI YA GEITA GOLD UWANJA WA MKAPA
Next articleKIKOSI CHA GEITA GOLD DHIDI YA SIMBA