Home Sports SITA WACHAGULIWA KAMATI YA MASHINDANO YANGA

SITA WACHAGULIWA KAMATI YA MASHINDANO YANGA

 RAIS wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said ameteua Wajumbe wa Kamati ya Mashindano Yanga

Injinia ameweza kuteua kamati hiyo kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ili kuweza kuunda kamati hiyo maalumu.

 Ni wajumbe 6 wametangazwa leo Agosti 10.2022 kuweza kuwa katika kamati hiyo kutimiza majukumu yao.

Ni pamoja na Mustapha Himba,Lucas Mashauri,Seif Ahmed,(Magari),Pelegrius Rutayunga,Davis Mosha na Majid Suleiman.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi huku nahodha akiwa ni Bakari Mwamnyeto kipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Agosti 13,Uwanja wa Mkapa.

Previous articleMSHAMBULIAJI WA KAZI ATAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA
Next articleTAREHE YA UFUNGUZI KOMBE LA DUNIA YARUDISHWA NYUMA