Home Sports MSHAMBULIAJI WA KAZI ATAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA

MSHAMBULIAJI WA KAZI ATAJWA KUINGIA RADA ZA YANGA

KUTOKANA na taarifa kueleza kuwa nyota wao Dario Federico yupo kwenye hesabu za kuondoka ndani ya Singida Big Stars timu hiyo imebainisha kuwa nyota huyo bado yupo ndani ya kikosi hicho.

Habari zimeeleza kuwa mshambuliaji huyo ambaye amekuwa kwenye mwendo mzuri wa kufanya vizuri katika mechi za hivi karibuni yupo kwenye hesabu za Yanga.

Yanga wanatajwa kuanza kufanya mazungumzo na staa huyo ili kuweza kuwa naye kwenye kikosi chao kimataifa msimu wa 2022/23.

Klabu ya Big Star kupitia kwa Ofisa Habari, Hussen Massanza wameweka wazi kuwa hakuna mpango wa nyota huyo kuondoka.

“Ni mchezaji wetu Dario Federico tupo naye hawezi kwenda sehemu yoyote kwa sasa ana mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hii ya wakulima,”.

Previous articleARSENAL YAMSAKA WINGA KWA PAUNDI 40
Next articleSITA WACHAGULIWA KAMATI YA MASHINDANO YANGA