Home Sports OKTOBA 23 NI SIMBA V YANGA KWA MKAPA

OKTOBA 23 NI SIMBA V YANGA KWA MKAPA

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) Almasi Kasongo Agosti 3, 2022 ametangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2022/2023 ambapo Klabu ya Yanga itafungua pazia lake la ligi hiyo kwa kuwa mgeni wa Polisi Tanzania.

Kwa upande wa Klabu ya Simba wao wataanza na Geita Gold FC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Yanga itacheza pambano lake hilo siku ya Agosti 16, 2022 huku wapinzani wao Simba wao wakimenyana na Geita Gold FC siku ya Agosti 17, 2022.

Aidha Kasongo amesema mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba utachezwa Oktoba 23, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 11 jioni.

Kuhusu ratiba ya Ligi Kuu ya NBC wakati wa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia, Kasongo amesema Ligi itaendelea kama kawaida licha ya kuwepo kwa mashindano hayo.

“Tunatarajia kuwa na michezo 240 ya mizunguko 30 kwa mizunguko 30 kwa msimu wa 2022/23,michezo ya mzunguko wa kwanza inapigwa Agosti 15 na ile ya mzunguko wa mwisho itachezwa Mei 27,2023,”.

Previous articleSIMBA YAMSHUSHA KIUNGO MNIGERIA,AZIZ KI,MAYELE WAKABIDHIWA SIMBA
Next articleMWAIKIMBA ASIMULIA ALIVYOLAMBA M 58 ZA M-BET TANZANIA